BAADHI ya wanachama wa klabu ya Yanga, wametoa mpya kwa kuwatakai watani zao, Simba kila la heri katika pambano lao la Ligi ya Mabingwa Afrika wakiitaka wasiipoteze nafasi waliyoipata baada ya kushinda ruifaa yao dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.
Iggawa wapo wana Yanga wengine wanaowakejeli Simba kuwa, wataishia kunawa katika pambano hilo litakalochezwa wiki ijayo dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco, bado baadhi wameitakia kila la heri timu hiyo ili iweze kupeperusha vema bendera ya Tanzania.
Mwanachama na mchezaji wa zamani wa Yanga, Ramadhani Kampira, alisema kuwa nafasi iliyopata Simba, inapaswa kutumiwa vema na watani zao hao kwa kuweza kuishinda Wydad na kuthibitisha kuwa walistahili kabisa kuendelea na michuano hiyo ya kimataifa.
"Binafsi naupongeza uongozi wa Simba kwa ufuatiliaji wa mambo, kilichobaki wachezaji kupigana kufa na kupona kuipa timu ushindi kwani hiyo ni nafasi adimu ambayo hawapaswi kuipoteza, naitakia kila la heri ili waipeperushe bendera ya Tanzania," alisema Kampira.
Kampira aliongeza kuwa, japo wapo wenzake wanaoikebehi Simba kwa kupata ushindi wa mezani, ila bado wanapaswa kutambua kuwa timu hiyo ni mwakilishi wa Tanzania na mafanikio yao ni ya Watanzania wote katika anga la kimataifa.
"Simba ni timu ya Tanzania, suala la ushindi wa mezani au la dio ishu kama kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za mashindano, kitu cha muhimu tuiombee ifanye vema ili sifa ziendelee kurudi Tanzania," alisema Kampira aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka wilaya ya Kinondoni, KIFA.
Hata hivyo Kampiora akisema hivyo mashabiki wengine wa klabu hiyo ya Jangwani,
wameonekana kuwa na 'donge' kwa kuipiga kijembe Simba kwamba hawataenda kokote zaidi ya kujitia aibu mbele ya Wydad na hata mpinzani wake wa Kombe la Shirikisho, DC Motema Pembe ya DR Congo kama itapoteza mechi dhidi ya waarabu hao.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alinukuliwa akisema wao wamejiandaa kufanya vema katika mechi hiyo wakishukuru CAF kuusogeza mchezo huo toka wiki hii hadi wiki ijayo, akidai itawasaidia kupata fursa nzuri ya kujiandaa na kusema wanaowabeza waendelee kubeza tu.
No comments:
Post a Comment