Tuesday, May 17, 2011

Tanzania Flava Unity waja na Miaka 50 ya Uhuru

KUNDI la Umoja wa Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya la Tanzania Flava Unity, TFU, linalojumuisha wasanii zaidi ya 100 wameibuka na wimbo mpya wa pamoja uitwayo Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, ambapo kazi ya kushuti video ya wimbo huo ulikuwa ukiendelea kufanywa leo kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kundi hilo, MwanaFA, alisema kibao cha wimbo huo ambao ulitambulishwa rasmi kama kwenye kipindi cha XXL cha Radio Cloud's FM, umeimbwa na wasanii 34, lakini video yake inashirikisha wasanii 50.
MwanaFA aliweka bayana kwamba kazi hiyo mpya imefanyiwa kazi na watayarishaji mahiri wa muziki nchini, Lamar na Makochal na video imepigwa na Visual Lab chini ya Mussa Adam.
Kazi hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa wasanii wa muziki huo kushirikiana kuachia kazi ya pamoja wakifuata mkondo uliowahi kufanywa na wanamuziki nyota duniani miaka ya 1980 walipoimba kibao cha 'We are the World' kuhamasisha mapambano dhidi ya Njaa Barani Afrika.
Baadhi ya vichwa vilivyoshiriki kwenye kazi hiyo ya TFU inayoongozwa na MwanaFA ambaye ni Mwenyekiti, huku Makamu wake akiwa ni TID, Katibu akiwa na Karapina na msaizidi wake, Lamar na wajumbe kadhaa kama Banana, Mwasiti, Chegge na wengine ni pamoja na Mr Blue, Madee, Tundaman, Cassim, Mheshimiwa Temba, Mwasiti, Keysher, TID, Godzillar, Dongo Janja na wakali wa miondoko yote nchini.

No comments:

Post a Comment