Monday, May 30, 2011
Roman Mng'ande: Mpuliza tarumbeta anayezeekea Msondo Ngoma
MASHABIKI wa Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' walimbatiza jina la 'Romario', wakifananisha utundu na umahiri wake wa jukwaani sawa na aliokuwa nao nyota wa zamani wa Brazil, Romario aliyekuwa mkali wa kufumania nyavu uwanjani.
Hata hivyo, hawakukosea kumpa jina hilo kutokana na ukweli kwamba, kabla ya kutumbukia kwenye muziki akikojifunza kupuliza tarumbeta kwa Father Kanuti, mjini Morogoro, Romario ambaye majina yake kamili ni Roman Mng'ande, alikuwa mahiri katika soka.
Mng'ande, aliyeitumikia Msondo karibu miaka 30 sasa, alisema enzi akisoma na hata alipoingia kwenye muziki alikuwa mshambuliaji wa kati, akifananishwa na nyota wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Sunday Manara 'Computer'.
"Kabla ya kuingia kwenye muziki, nilikuwa namba 9 hatari nikizichezea timu za Kilakala Stars na timu ya mkoa wa Morogoro katika Taifa Cup, miaka ya 1970," alisema.
"Hata nilipokuja Dar kujiunga Urafiki Jazz mwaka 1980 na nilipotua Juwata niliendelea kucheza nikiwa na timu ya Mwanga All Stars hadi nilipostaafu 1987." aliongeza.
Mng'ande aliyeanza fani za sanaa na michezo tangu akiwa shule ya msingi, alisema alipenda muziki kutokana na kuvutiwa na marehemu Mbaraka Mwinshehe na kurithi kipaji toka kwa wajomba na mama yake.
Alisema, mama yake mzazi ambaye ni marehemu kwa sasa alikuwa mahiri kwa uimbaji wa nyimbo asilia, huku wajomba zake wakipiga magitaa ya kienyeji (galaton) katika shoo za klabu za pombe.
Alisema alichukuliwa na Father Kanuti mwaka 1973, kuendeleza kipaji chake cha kupuliza filimbi alichokianza akiitumikia bendi ya shule na alipohitimu alipiga bendi kadhaa za mtaani wa Morogoro kabla ya kufuatwa na Urafiki Jazz mwaka 1980.
Mwaka mmoja baadaye aliihama Urafiki na kujiunga na Tanzania Stars iliyokuwa ikitumbuiza kwenye ukumbi wa Magoti enzi hizo, kisha kutua Msondo Ngoma enzi ikiitwa Juwata Jazz mwaka 1982 na kibao cha kwanza kukishiriki kikiwa ni 'Faulata'.
Tangu wakati huo hadi leo Mng'ande hajahama Msondo. Ameshiriki albamu zote za bendi hiyo tangu mwaka huo, akiwa ni mmoja wa viongozi na pia rapa.
Kuhusu mafanikio, Mng'ande alisema muziki umemfanya ajenge nyumba tatu, zilizopo Keko Mwanga, Kibamba na Chanika, pia anamiliki mashine za kuchomea vyuma, vyerehani na kuitunza familia yake na kuwasomesha watoto wake.
Mkongwe huyo ana watoto wanne aliozaa na mkewe Letcia Francis aliyeoana naye mwaka 1981, ambao ni Jenifer Mng'ande (28), Daktari anayefanya kazi hospitali ya Mahenge, Morogoro na Stella Mng'ande (25) anajishughulisha na biashara.
Wengine ni Chriss (17) anayejiandaa kumaliza kidato cha nne ambaye pia ni dereva na Rich (10) anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Airwing, Ukonga Dar es Salaam.
Mng'ande alisema hatarajii wanae kumrithi kipaji cha muziki kwa vile amewazuia kujihusisha.
Shabiki huyo wa klabu ya Yanga na Arsenal ya Uingereza, anamzimia mpiga solo, Said Mabela 'Dokta' aliyenaye Msondo Ngoma, akidai ni mwanamuziki anayeujua muziki.
"Huyu jamaa achana naye, anaujua muziki, sisi tuliye karibu 'tunainjoi'. Alistahili kupewa tuzo ya heshima na Kili Music Awards-2011."
Mng'ande, aliyezaliwa Februari 7, 1964 mjini Morogoro akiwa ni mtoto wa tatu kati ya wanne wa Mzee Mng'ande, alisema hakuna tukio la furaha kwake kama lile la mwaka 1979 aliposhikana mkono na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Nyerere.
"Tukio hilo lililotokea tulipoenda kuzima Mwenge huko Butiama, litabaki kichwani hadi milele yote kwa vile ni jambo ambalo sikulitarajia," alisema.
Juu ya huzuni, Mng'ande alisema ni kuwapoteza wazazi wake wawili, hasa kushindwa kumzika mama yake mwaka 1990. Baba yake alifariki miaka mitatu baadaye.
"Kushindwa kumzika mama kutokana na kukosekana kwa mawasiliano nikiwa Dar kunaniuma hadi leo, ila naamini yote ilikuwa ni mipango ya Mungu tu," alisema.
Mng'ande, anayependa kula Ugali kwa Samaki, kinywaji chake kikiwa ni soda, alisema kama angekutana na rais angemuomba aweke sera za kupunguza ushuru na kodi kwa vyombo vya muziki ili kurahisisha upatikanaji wake na kusaidia wengi kujiajiri.
"Vyombo vya muziki vipo juu na kuwakwaza wengi kuvimiliki, ila mimi ningekuwa rais ningeinua uchumi na kuinua maisha ya wananchi nikiboresha huduma muhimu kama za Afya, Elimu na Kilimo," alisema.
Kuhusu kuporomoka kwa muziki wa dansi, Mng'ande aliyekitaja kibao cha 'Kilio cha Mtu Mzima' kama moja ya kazi ya kujivunia kwake kwa jinsi alivyoitendea haki, alisema hali hiyo inatokana na bendi nyingi kuendekeza tabia ya kuiga kazi za nje.
"Muziki wetu unaporomoka kwa sababu bendi nyingi zinaiga kazi za wanamuziki wa nje na kuwafanya mashabiki watususe kwa kutoona tofauti," alisema.
Tabia ya baadhi ya wanamuziki wameshafika mbali wakati ndio kwanza wanaanza imechangia muziki wa dansi kupoteza kasi yake ya awali.
"Bongofleva nawasifu kwa mafanikio, ila wana tatizo la kuwa wavivu kujifunza kupiga ala ili kwenda na wakati na kukamilika kuwa wanamuziki.
Alisema mazoea ya kupiga muziki kwa kutumia 'Play Back' hautawafikisha kokote.
Mbwana: Sitamsahau Mfilipino aliyening'oa jino ulingoni
KIPAJI chake cha ngumi kilichoanza kuonekana tangu akiwa kinda akirithi kutoka kwa baba na kaka zake, kilimwezesha Mbwana Matumla 'Golden Boy' kupata ajira bila kutarajia ndani ya Jeshi la Polisi mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Bondia huyo maarufu anayeshikilia taji la Ubingwa wa Mabara wa UBO, uzani wa Superfly, alivutwa Polisi tangu akiwa yupo darasa la tano katika Shule ya Msingi Mgulani.
Alisema alichukuliwa na Polisi ili kuichezea timu yao na ngumi na alipomaliza masomo yake ya msingi alipewa ajira mwaka 1993.
Miaka miwili baadae alipelekwa kwenye shule ya uaskari ili kuwa askari kamili, wakati ambao alikuwa tayari alishaisaidia timu hiyo kutamba katika ngumi, huku mwenyewe akijijengea jina anga za kimataifa.
"Huwezi amini niliajiriwa Polisi kama utani baada ya kuwavutia kwa kipaji changu, nakumbuka nilichukuliwa nikiwa darasa la tano, lakini niliajiriwa mwaka 1993 kabla ya kupelekewa 'depo' mwaka 1995," alisema.
Mbwana, aliyetwaa mataji mbalimbali katika ngumi za ridhaa akiwa na Polisi na timu ya Taifa, alisema hata hivyo alilazimika kuacha ajira jeshini mwaka 1997 baada ya kushawishiwa kuingia katika ngumi za kulipwa zilizompa mafanikio zaidi kimaisha.
"Niliacha kazi Polisi mwaka 1997 na kutumbukia kwenye ngumi za kulipwa kwa ushawishi wa kocha, Norman Hlabane, wa Afrika ya Kusini, aliyekuwa akimnoa kaka Rashid, ndiye aliyenipa hili jina la 'Golden Boy' kwa kukunwa na ukali wangu," alisema.
Mbwana, alisema alipanda ulingoni kwa mara ya kwanza katika ngumi za ridhaa katika michuano ya wazi na kumpiga Abdul Mgweno aliyeichezea klabu ya Urafiki.
Aliendelea kutamba akiwapiga wapinzani wake na kuteuliwa kwenye timu ya taifa, ambapo aliisaidia kuiletea sifa Tanzania kwa kutwaa medali kadhaa kwenye michuano mbalimbali kabla ya kuhamishia makali yake kwenye ngumi za kulipwa.
Mbwana alilitaja pambano la kwanza kwa ngumi za kulipwa kwake lilikuwa dhidi ya Mussa Njeu aliyempiga kwa KO, raundi ya kwanza na kuingia moja kwa moja kwenye orodha ya mabondia wa Kanda ya Tano mwaka huo wa 1997.
Taji la kwanza kimataifa kwake ni mkanda wa WBU-International alipomchakaza kwa KO ya raundi ya kwanza bondia wa Hungary, Tamas Szakallas, katika pambano lililofanyika Tanzania, Desemba 19, 1998.
Mataji mengine aliyowahi kutwaa ni WBA, WBN, PABA, WBU, ICB, IBO na UBO anaoushikilia hadi sasa ambapo aliutwaa mara ya kwanza mwaka 2009 kwa kumpiga Mganda, Festus Omondi, na kutetea hivi karibu mbele ya Mkenya Gabriel Ochieng.
Mbali na mikanda hiyo, Matumla, ambaye ni mnazi mkubwa wa timu ya Simba na klabu ya Manchester United ya Uingereza iliyofungwa 3-1 na Barcelona katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa usiku wa kuamkia jana, amewahi kutwaa tuzo mbalimbali ikiwemo ile ya Mwanamichezo Bora inayotolewa na TASWA mwaka 1993 na 1998, Shujaa wa Taifa mwaka 2000 na ile ya Guinness Book.
MFILIPINO
Licha ya kucheza mapambano mengi ya ngumi, Mbwana alisema pambano dhidi ya Mfilipino, Joel Avala, lililofanyika Machi 30, 2001 jijini Dar es Salaam ndilo gumu na lisilosahaulika kichwani mwake.
Alisema hawezi kulisahau pambano hilo gumu ambalo licha ya kushinda, alipoteza jino lake lililong'oka bila ganzi ulingoni baada ya mpinzani wake huyo kumpiga kichwa mdomoni.
"Siwezi kulisahau pambano dhidi ya Joel Avala kwa jinsi lilivyokuwa gumu na kitendo cha kung'oka jino ulingoni kisha kumchakaza mkali huyo kwa kumshinda katika raundi ya saba... kumbuka alikuwa mzoefu kuliko mimi," alisema.
Alitaja pambano jingine gumu kwake ni dhidi ya Edison Torres wa Venezuela aliyempiga mbele ya mashabiki wake na kuunganisha mataji ya WBA-Afrika na la Latin America.
Mbwana, aliyeoana na Susan Rashid na kuzaa nae watoto watatu, Mariam (17), aliyepo kidato cha tatu Shule ya Sekondari Wailes - Temeke, Leila (8), aliyepo darasa la pili Shule ya Msingi Mgulani na Yusuf (1), alimshukuru kocha Habib Kinyogoli kumfikisha alipo.
"Huyu ndiye aliyekuza kipaji changu, licha ya kwamba pia nimepitia mikononi mwa makocha wengine kama Norman Hlabane, Kinyogoli ana mchango mkubwa kwangu na ngumi za Tanzania," alisema.
Mbwana aliyelitaja tukio la kupata mtoto wa kiume (Yusuf) kuwa ndilo la furaha mwake, alisema kucheza kwake ngumi kumemsaidia mengi kama kujenga nyumba mbili, kumiliki kiwanja Ukonga, jijini Dar es Salaam na kuendesha shughuli za biashara.
"Pia, nimeijua dunia kupitia ngumi, nina marafiki wengi, kifupi ngumi zimenisaidia sana," alisema.
Mbwana anayependa kula ndizi kwa nyama na soda aina ya Fanta, alisema mchezo wa ngumi nchini umedorora sasa kwa kuwepo migogoro na kukosekana kwa wadhamini, akidai angekutana na Rais hicho ndicho kingekuwa kilio chake kwake.
"Ngumi zimetelekezwa licha ya kuitangaza nchi kwa kutoa mabingwa wa dunia, hivyo ningemuomba Rais asaidie ziwe na wadhamini kama alivyofanya katika soka," alisema.
Na kama yeye Mbwana angekuwa angekuwa Rais wa nchi hii, angeboresha huduma zote za jamii, akihakikisha rasilimali za nchi zinasaidia kuinua uchumi kuwanufaisha wananchi wote, pia kusaidia kuinua michezo ili kusaidia ajira kwa wengi.
Mbwana anayekunwa na Floyd Mayweather Jr. kwa umahiri wake wa kutupa ngumi ulingoni, amepanga kustaafu ngumi miaka mitano ijayo ili awe kocha wa mchezo huo.
"Nimepanga kustaafu miaka mitano ijayo niwe kocha kuinua nyota wapya, tayari nimeshaianza kazi hiyo nikishirikiana na kaka Rashid."
Mbwana Ally Matumla, alizaliwa Aprili 8,1975, Dar es Salaam. Ni mtoto wa tano kati ya watoto 11 wa Mzee Ally Matumla, alisoma Shule ya Msingi Mgulani na kujihusisha katika michezo hasa soka, sarakasi kabla ya kugeukia ngumi hadi leo.
Bangkok Deal sasa ni Bangkok Dream
SEHEMU ya pili ya filamu ya kutisha ya 'Bangkok Deal' ipo hatua ya mwisho kabla ya kuachiwa
mitaani ikibadilishwa jina na kuitwa 'Bangkok Dream'.
Mkurugenzi wa kampuni ya Huba Film Production, Husseni Ramadhani 'Swagger One' alisema sababu ya kuipa filamu hiyo jina jipya ni kujitofautisha na watayarishaji wengine waliozoea kuendeleza jina la filamu hata katika matoleo zaidi ya mawili.
Swagger, aliyewahi kutamba kwenye muziki na filamu kabla ya kugeukia utayarishaji, alisema
ameona kurejea jina la 'Bangkok Deal' hata katika sehemu hiyo ya pili ni 'ukale' ambao wengine
wanapaswa kufuata mkondo wake.
"Bangkok Dream ni muendelezo wa Bangkok Deal, ila nimeipa jina jipya kuonyesha mfano kwa wengine kuacha kuendekeza 'ukale' wa kutoa filamu kwa jina moja katika sehemu hata nne, hali inayochosha watazamaji wetu." alisema.
Aliongeza filamu hiyo iliyokuwa ikipigwa picha zake eneo la Kigamboni, nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam, imekamilika na sasa inafanyiwa uhariri kabla ya kuingizwa sokoni.
Swagger aliyetamba na kundi la Crime Buster, lenye wasanii kadhaa akiwemo Blandina Chagula 'Johari', Renatus Pamba 'Mr Simple' ambaye kwa sasa ni Diwani wa Sinza na Saleh Komba 'Mourin', alisema kazi hiyo mpya ni 'funika bovu' kwa jinsi washiriki walivyoonyesha kiwango, kuliko hata toleo la awali.
"Ninachoomba, wadau wa filamu waisubiri iingie sokoni wapime maelezo yangu, ila ni kazi yenye kiwango cha hali ya juu pengine kuliko 'Bangkok Deal' ambayo ipo kwenye mchakato wa kushirikishwa kwenye Tamasha la Kimataifa la filamu za Zanzibar, ZIFF," alisema.

Chumo kuzinduliwa bure j'mosi
FILAMU mpya ya kimataifa ya 'Chumo' inatarajiwa kuzinduliwa bure kwenye viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar es Salaam, siku ya Jumamosi uzinduzi utakaosindikizwa na makundi ya muziki ya Ashimba na Jagwa Music.
Uzinduzi wa filamu hiyo inayohusiana na masuala ya mapenzi, lakini yenye kuelimisha juu ya ugonjwa wa Malaria hasa kwa Wajawazito na watoto, utafanyika saa chache baada ya kuachiwa rasmi mitaani siku hiyo hiyo ya Jumamosi.
Taarifa toka kwa wasambazaji wa filamu hiyo iliyoshinda tuzo za Golden Hamster katika tamasha la filamu la Northwest Projections, Marekani, kampuni ya Steps Entertainment ni kwamba filamu hiyo itaachia rasmi mitaani siku hiyo na jioni yake itazinduliwa rasmi bure.
"Filamu ya Chumo, ambayo inatarajiwa kuingia mitaani siku ya Jumamosi itazinduliwa rasmi siku hiyo hiyo jioni kwenye viwanja vya Biafra, wakisindikizwa na makundi ya muziki ya Ashimba na Jagwa Music, bila kiingilio chochote," taarifa hiyo ya Steps ilisema.
Filamu hiyo iliyoteuliwa kwenye matamasha ya filamu ya ZIFF, Pan African na Durban International Films Festival, imewashirikisha wasanii kadhaa nyota nchini akiwemo Miss Temeke-2006, Jokate Mwegelo, Yusuph Mlela 'Angelo', Hussein Mkiety na Jafaki Makatu.
Kazi hiyo mpya iliyotararishwa na Jordan Ribery imetayarishwa nchini na Asasi ya MFDI-Tanzania na kufadhiliwa na JHU-CCP kupitia Mfuko wa Rais wa kutokomeza Malaria na Shirika na Misaada la Marekani, USAID.

Tuesday, May 17, 2011
Visura Miss Bagamoyo 2011 kambini
VISURA waliojitokeza kushiriki shindano la kumsaka mrembo wa mji wa Bagamoyo, 'Vodacom Miss Bagamoyo-2011' wameingia kambini tangu wiki iliyopita tayari kujiandaa na shindano hilo litakalofanyika Mei 28.
Warembo hao 12 wameingia kambini kwenye ukumbi wa New Mzalendo Pub, uliopo jengo la Millenium Tower, jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa onyesho hilo, Awetu Salim, alisema wameamua kuiweka kambi hiyo jijini ili kuwapa urahisi warembo waliojitokeza kushiriki shindano hilo ambalo litafanyikia kwenye ukumbi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo, TaSUBA, mjini Bagamoyo.
Awetu, alisema karibu asilimia kubwa ya warembo waliojitokeza licha ya kutokea Bagamoyo, lakini shughuli zao nyingi huzifanya Dar es Salaam ambapo wanafanya kazi au kusoma.
"Warembo wetu wameingia kambini kwenye ukumbi wa New Mzalendo Pub, uliopo eneo la Makumbusho, tayari kujiandaa na shindano la Mei 28," alisema Awetu.
Mratibu huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Asilia Decoration, hakuweza kuwataja majina ya visura hao kwa madai, hakuwa na orodha wakati akizungumza na mtandao huu..
"Wapo warembo zaidi ya 12 na tayari wameshanza kunolewa wakipewa mbinu za kuweza kuinuka washindi wa kinyang'anyiro hicho, cha Vodacom Miss Bagamoyo 2011," alisema Awetu.
Awetu alisema katika onyesho lao hilo litapambwa na burudani kamambe toka kwa kundi mahiri la muziki wa taarab la Jahazi Modern 'Wana Naksh Naksh' linaloongozwa na 'Mfalme' Mzee Yusuph.

Handsome wa Ray huyoooo!
FILAMU mpya ya msanii nyota wa fani hiyo nchini, Vincent Kigosi 'Ray', iitwayo 'Handsome wa Kijiji', imekamilika na sasa ipo katika maandalizi ya kuachiwa mitaani.
Kwa mujibu wa taarifa toka kwa wasambazaji wa filamu hiyo kampuni ya Steps Entertainment, ni kwamba kazi hiyo ya Ray ipo kwenye foleni ikisubiri zamu yake ya kuachiwa mtaani.
"Kazi mpya ya Ray iitwayo 'Handsome wa Kijiji' imekamilika na tayari imewekwa kwenye foleni kwa ajili ya kuandaliwa kuachiwa mtaani, ni moja ya kazi bomba sana na ambayo inamtoa Ray kivingine," taarifa hiyo ya Steps inasomeka hivyo.
Filamu hiyo ambayo kwa mara ya kwanza itamuonyesha Ray akicheza kama mtu duni akiwa kijijini, tofauti na kazi zake nyingi ambazo amekuwa akiigiza kama tajiri na mtoto wa mjini tu.
Ray katika taarifa yke ya awali kabla ya kwenda kuirekodi filamu hiyo, alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na maombi ya mashabiki wake waliodai walikuwa wamekinaishwa nae kumuona kila siku akiigiza mjini na hivyo kwenda Bagamoyo kuiandaa filamu hiyo.
Ndani ya filamu hiyo, Ray ameshiriki na wasanii chipukizi na wakongwe ambao wameinogesha, baadhi wakiwa ni Irene Paul, Vailet Nestory, Flora Mvungi, Ben Branco, Mzee Magali, Hashim Kambi, Tash na wengineo.
Taarifa hiyo inasema kuwa, filamu hiyo huenda ikaachiwa mwishoni mwa mwezi huu pamoja na kazi nyingine ambazo zipo kwenye foleni.

Vimwana wa Twanga Pepeta 'kufundwa'
VIMWANA waliojitokeza kushiriki shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011, wameanza kupata mafunzo ya ujasiriamali yanayolenga kuwapa ujuzi wa kuendesha biashara mbalimbali.
Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo, Maimatha Jesse, vimwana 23 wamejitokeza kuwania taji hilo, ambapo kwa sasa wanaendelea kujifua chini ya mkufunzi wao 'Super K' na Matron Husna Idd 'Sajent'.
"Shindano la mwaka huu mshindi atazawadiwa duka la vipodozi, ndio maana tumewaletea wataalam wa mambo ya biashara ambao huwapa mafunzo ya ujasiriamali vimwana wetu," alisema Maimatha.
Maimatha alisema, kutokana na zawadi hiyo, vimwana hao wamekuwa wakifanya mazoezi, kisha kupewa elimu hiyo ambayo anaamini itawasaidia sio tu kwenye shindano hilo bali pia katika shughuli zao binafsi.
Alifafanua, zawadi za washindi wa tatu na wa nne zitatangazwa mara baada ya kufanyika shindano la nusu fainali ambalo litabakiza vimwana 10 tu kati ya hao 23 wanaoendelea na mazoezi sasa.
Maimatha alisema, shindano la nusu fainali litafanyika Mei 27 ndani ya ukumbi wa Club Sun Cirro, Sinza Dar es Salaam na vimwana 10 watakaobaki ndio watachuana kwenye fainali.
Fainali za michuano hiyo zitafanyika Juni 3, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kama mipango yao itaenda vema.

Wagombea Villa Squad 'kikaangoni' Jumamosi
WAGOMBEA 14 waliojitokeza kuwania nafasi ya uongozi ndani ya klabu ya Villa Squad wanatarajiwa kufanyiwa usaili wao kesho kabla ya kuanza mbioni za kujinadi kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Juni 12.
Awali uchaguzi huo ulitangazwa ungefanyika Mei 22, lakini kwa mujibu wa makubaliano baina ya Kamati za Uchaguzi za Villa na TFF, uchaguzi huo sasa utafanyika katika tarehe hiyo mpya.
Katibu wa Kamati ya Uchaguzi wa Villa, Frank Mchaki, aliuambia Mtandao huu kuwa, jumla ya wagombea 14 wamejitokeza kuwania nafasi za uongozi katika klabu hiyo ambao kesho watasailiwa kupitisha majina ya watakaochuana kwenye uchaguzi mkuu mwezi ujao.
Alisema kwenye nafasi ya Uenyekiti yupo mgombea mmoja tu, ambaye ni Abdalla Majura Bulembo, huku kwenye nafasiu ya Umakamu Mwenyekiti kuna wagombea wawili wanaowania nafasi hiyo na waliosalia ni wanaozitaka nafasi saba za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
"Usaili wa wagombea wetu utafanyika Mei 21 ambapo watakaokidhi vigezo na sifa watapitishwa kabla ya kusubiri kama kuna mapingamizi yatakayowekwa, kisha wagombea kuanza kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Juni 12," alisema Mchaki.
Villa itafanya uchaguzi huo wiki moja kabla ya kuanza rasmi kwa zoezi la usajili wa wachezaji kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo timu hiyo ni miongoni mwa klabu mpya nne zilizopanda daraja toak Ligi Daraja la Kwanza.
Timu nyingine zilizopanda daraja na Villa ni JKT Oljoro ya Arusha, Coastal Union ya Tanga na Moro United ya Dar es Salaam.

Muumin amuonya Banza Extra Bongo
MWIMBAJI nyota wa muziki wa dansi nchini, Mwinjuma Muumin 'Kocha wa Dunia',
amemuonya mwanamuziki mpya wa Extra Bongo, Ramadhani Masanja 'Banzastone'
akimwambia kama anataka kujiletea mabadiliko kimuziki lazima aachane na masuala ya Ulevi.
Pia, Muumin, alisema kitendo cha Banza kujiunga Extra Bongo kinafanana na alivyowahi kufanya yeye alipojiunga na Ally Choki na kuunda bendi ya Double Extra, ambapo Banza aliifananisha hatua hiyo sawa na kutengeneza kitanda kwa kuunganisha stuli na meza.
Akizungumza na Mtandao huu, Muumin alisema Extra Bongo inaweza kunufaika zaidi na ujio wa Banza endapo mkali huyo ataachana na ulevi na mambo mengine yaliyoshusha kimuziki.
"Kila mdau wa muziki wa dansi ukimuuliza ategemee nini juu ya kuungana kwa Choki na Banza pale Extra Bongo, kwanza atatarajia kusikia makubwa kutoka kwa wanamuziki hao, lakini akitafakari jinsi Banza anavyosumbuka na ulevi, bila shaka atakata tamaa," alisema.
Alifafanua, katika mazingira ya kawaida Banza ni mwanamuziki mkali na nyota lakini siyo siri kuwa ukali wake unaathiriwa na ulevi unaomsababishia ajisahau hivyo kupotea umakini.
Banza alitangaza kujiunga na Extra Bongo wiki chache zilizopita na tayari ameshaizawadia wimbo mpya bendi hiyo unaojulikana kama 'Falsafa' ambao wapenzi wa muziki walipata fursa ya kuusikia 'live' jukwaani wamesifu maneno yaliyotumika na kuonyesha kuwa bado wamo.
Muumin ambaye kwa sasa anaitumikia bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', alisema hataki kuwa mtabiri wa maisha ya watu katika fani, ila anaamini endapo Banza hataacha ulevi ndoto yake ya kuisaidia Extra Bongo itabaki kuwa kitendawili kisichoteguka.

Yanga waipongeza Simba 'ushindi wa mezani'
BAADHI ya wanachama wa klabu ya Yanga, wametoa mpya kwa kuwatakai watani zao, Simba kila la heri katika pambano lao la Ligi ya Mabingwa Afrika wakiitaka wasiipoteze nafasi waliyoipata baada ya kushinda ruifaa yao dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.
Iggawa wapo wana Yanga wengine wanaowakejeli Simba kuwa, wataishia kunawa katika pambano hilo litakalochezwa wiki ijayo dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco, bado baadhi wameitakia kila la heri timu hiyo ili iweze kupeperusha vema bendera ya Tanzania.
Mwanachama na mchezaji wa zamani wa Yanga, Ramadhani Kampira, alisema kuwa nafasi iliyopata Simba, inapaswa kutumiwa vema na watani zao hao kwa kuweza kuishinda Wydad na kuthibitisha kuwa walistahili kabisa kuendelea na michuano hiyo ya kimataifa.
"Binafsi naupongeza uongozi wa Simba kwa ufuatiliaji wa mambo, kilichobaki wachezaji kupigana kufa na kupona kuipa timu ushindi kwani hiyo ni nafasi adimu ambayo hawapaswi kuipoteza, naitakia kila la heri ili waipeperushe bendera ya Tanzania," alisema Kampira.
Kampira aliongeza kuwa, japo wapo wenzake wanaoikebehi Simba kwa kupata ushindi wa mezani, ila bado wanapaswa kutambua kuwa timu hiyo ni mwakilishi wa Tanzania na mafanikio yao ni ya Watanzania wote katika anga la kimataifa.
"Simba ni timu ya Tanzania, suala la ushindi wa mezani au la dio ishu kama kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za mashindano, kitu cha muhimu tuiombee ifanye vema ili sifa ziendelee kurudi Tanzania," alisema Kampira aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka wilaya ya Kinondoni, KIFA.
Hata hivyo Kampiora akisema hivyo mashabiki wengine wa klabu hiyo ya Jangwani,
wameonekana kuwa na 'donge' kwa kuipiga kijembe Simba kwamba hawataenda kokote zaidi ya kujitia aibu mbele ya Wydad na hata mpinzani wake wa Kombe la Shirikisho, DC Motema Pembe ya DR Congo kama itapoteza mechi dhidi ya waarabu hao.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alinukuliwa akisema wao wamejiandaa kufanya vema katika mechi hiyo wakishukuru CAF kuusogeza mchezo huo toka wiki hii hadi wiki ijayo, akidai itawasaidia kupata fursa nzuri ya kujiandaa na kusema wanaowabeza waendelee kubeza tu.

Waydad mtihani mgumu kwa Basena
PAMBANO la mkondo mmoja wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya timu yake dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco, linatarajiwa kuwa kipimo tosha cha uwezo wa kocha mpya wa Simba, Mosses Basena kutoka Uganda.
Basena, aliyetua Simba kumrithi Mzambia, Patrick Phiri, anatarajiwa kuiongoza Simba katika mechi hiyo itakayochezwa wiki ijayo kwenye uwanja huru, ambapo wadau wa klabu hiyo watataka kuona kama ataivusha kwenda hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Afrika.
Kocha huyo aliyekuwa akiinoa timu ya taifa ya Uganda kama kocha msaidizi, hilo litakuwa ni pambano lake la kwanza kuiongoza Simba kwenye michuano yoyote tangu aliposaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa timu hiyo mapema mwezi huu.
Simba ilipata fursa ya kuumana na Waydad baada ya kushinda rufaa yake iliyokata Shirikisho la Soka Afrika, CAF, dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi wa Afrika, TP Mazembe ya DR Congo iliyokuwa imezitung'oa timu zote hizo mbili kwenye michuano hiyo ya Afrika.
Kupata fursa hiyo ya kucheza pambano hilo, Simba inayoendelea kujifua chini ya Basena, aliyekatisha mapumziko yake na kuanzisha programu maalum kwa ajili ya kuiweka vema timu hiyo, inapaswa kushinda ili kudhihirisha kuwa 'ngekewa' iliyoipata ilikuwa ni haki yao kwelikweli.
Licha ya kwamba hata kama timu yao itafungwa na wapinzani wao, bado itaendelea kucheza mechi za kimataifa kwa kushiriki Kombe la Shirikisho, wadu wengi wa Msimbazi wangependa kuona Simba ikifuzu hatua hiyo ili kuwaziba midomo watani zao wanaowakejeli mitaani.
Yanga, ambao awali waliibeza Simba kwa kusumbuka kukata rufaa hiyo, hivi sasa wameibuka upya wakikejeli nafasi iliopata watani zao kwa kudai itaishia 'kunawa' mbele ya Waydad, hivyo wana Msimbazi wangependa kuona kocha wao mpya akiwapa raha.
Basena, anayeendelea kuwafua wachezaji kwa mazoezi kabambe, tayari ameanza kuonyesha sio kocha wa mchezo na huenda akaisaidia Simba sio kwenye michuano hiyo ya kimataifa, bali hata kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo msimu huu walipoteza taji kwa watani zao, Yanga.
Hii inatokana na jinsi anavyowanoa wachezaji wake kwenye uwanja wa Taifa, akiwaweka tayari kukabiliana na Waarabu hao ambao hawana rekodi ya kutisha barani Afrika kama timu zingine za ukanda huo wa Afrika Kaskazini.

Deo Shija ana Jumba Bovu
MSANII nyota wa fani ya filamu nchini, DEogratius Shija, ameibuka na filamu mpya iitwayo Jumba Bovu, ikiwa miezi kadhaa tangu alipotamba na Imekula Kwangu.
Shija anayesifiwa kwa kutunga filamu zake na kuzipa majina ya kiswahili, ameweka bayana kwamba kazi yake hiyo mpya inawaibua wasanii wapya kama afanyavyo kwenye kazi zake zilizopita, safari hii akiiwatoa Margaret Akoonay na Neema Daniel alioshirikiana nae ndani ya kazi hiyo alichocheza pia na Simon Mwakangata.

Tanzania Flava Unity waja na Miaka 50 ya Uhuru
KUNDI la Umoja wa Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya la Tanzania Flava Unity, TFU, linalojumuisha wasanii zaidi ya 100 wameibuka na wimbo mpya wa pamoja uitwayo Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, ambapo kazi ya kushuti video ya wimbo huo ulikuwa ukiendelea kufanywa leo kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kundi hilo, MwanaFA, alisema kibao cha wimbo huo ambao ulitambulishwa rasmi kama kwenye kipindi cha XXL cha Radio Cloud's FM, umeimbwa na wasanii 34, lakini video yake inashirikisha wasanii 50.
MwanaFA aliweka bayana kwamba kazi hiyo mpya imefanyiwa kazi na watayarishaji mahiri wa muziki nchini, Lamar na Makochal na video imepigwa na Visual Lab chini ya Mussa Adam.
Kazi hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa wasanii wa muziki huo kushirikiana kuachia kazi ya pamoja wakifuata mkondo uliowahi kufanywa na wanamuziki nyota duniani miaka ya 1980 walipoimba kibao cha 'We are the World' kuhamasisha mapambano dhidi ya Njaa Barani Afrika.
Baadhi ya vichwa vilivyoshiriki kwenye kazi hiyo ya TFU inayoongozwa na MwanaFA ambaye ni Mwenyekiti, huku Makamu wake akiwa ni TID, Katibu akiwa na Karapina na msaizidi wake, Lamar na wajumbe kadhaa kama Banana, Mwasiti, Chegge na wengine ni pamoja na Mr Blue, Madee, Tundaman, Cassim, Mheshimiwa Temba, Mwasiti, Keysher, TID, Godzillar, Dongo Janja na wakali wa miondoko yote nchini.

Bangkok Dream yaiva
TOLEO la pili la filamu ya Bangkok Deal iliyopewa jina la Bangkok Dream inatarajiwa kuanza kupigwa picha wiki hii, chini ya jopo la wataalam toka kampuni ya Huba Films Production Next Vision.
Mkurugenzi wa kampuni ya Huba, Husseni Swagger, amesema mapema leo asubuhi kwamba kazi ya kushoot filamu hiyo mpya itaanza wakatyi wowote kuanzia leo.
Swagger, alisema wasanii wakaoshiriki kazi hiyo mpya tayari wameanza maandalizi ya kwenda location kwa ajili ya kuanza kazi, ili kuwapa burudani mashabiki wa filamu waliovutiwa na toleo la kwanza la filamu hiyo.
"Maandalizi kwa ujumla wa kuachia kazi mpya ya Bangkok Dream yameanza na nadhani kesho au keshokutwa tutaingia location kwa ajili ya kufyatua filamu hii," alisema Swagger.

Friday, May 6, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)