Sunday, April 24, 2011
Sikinde wana mbili mpya
BENDI ya Mlimani Park 'Sikinde' imekamilisha vibao viwili ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kujipanga upya baada ya kuondokewa na mwanamuziki wake, Shaaban Dede aliyejiunga na mahasimu wao, Msondo Ngoma.
Katibu wa bendi hiyo, Hamis Milambo, alisema kuwa bendi yao ambayo kwa wiki mbili mfululizo imekuwa kambini ikijifua, ambapo imekamilisha nyimbo mbili zilizotungwa na muimbaji wao mkongwe, Hassani Bitchuka.
"Tumeanza kujipanga upya kwa ajili ya kupakua albamu mpya na tayari tupo kambini kwa wiki ya pili sasa, ambapo tumeshakamilisha nyimbo mbili mpya zilizotungwa na Bitchuka," alisema.
Katibu huyo alisema nyimbo hizo zinazoendelea kufanyiwa mazoezi, hazijapewa majina hadi sasa na zitatambulishwa kwa mashabiki wao katika maonyesho yao ya Sikukuu ya Pasaka.
"Tutazitambulisha kwenye maonyesho yetu ya Pasaka, na hapo ndipo zitakapofahamika majina yake, ila ni kati ya nyimbo zitakazothibitisha kuwa Sikinde ni mabingwa wa muziki wa dansi nchini," alisema Milambo.
Milambo, alisema baada ya maonyesho ya sikukuu hiyo, bendi yao itakaa chini kufanyia mazoezi nyimbo nyingine ambazo zimeandikwa na waimbaji wao, Abdallah Hemba na Hamis Kunyata ili kuweza kukamilisha albamu yao ambayo wamepania kutoa kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.
Sikinde kwa sasa inatamba na albamu ya Supu Imetiwa Nazi, iliyotoka mwaka juzi na tangu hapo imekuwa ikiachia singo moja moja ukiwemo ule wa Wanawake Wanaweza na Tunu ya Upendo zilizokuwa zimetungwa na Shaaban Dede 'Mzee wa Loliondo' ambaye kwa sasa yupo Msondo Ngoma.
Kitabu cha Assosa chaingia mtaani
KITABU cha mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi, Tshimanga Kalala Assosa, kiitwacho 'Jifunze Lingala' kimeingia mitaani, huku mwenyewe akijiandaa kutoa toleo la pili la kitabu hicho kinachofundisha lugha ya Kilingala na Kiswahili.
Akizungumza na mtandao huu, Assosa, alisema kitabu hicho ambacho mbali na kufunza watu Kilingala, pia kina tafsiri ya nyimbo za wanamuziki maarufu wa Kongo na kiliingia sokoni tangu juzi huku kikigombewa kama njugu.
Assosa, alisema tangu akiingize sokoni kitabu hicho kimeshauza kopi zaidi ya 1000, huku akipokea oda kedekede toka kila pembe ya nchi kwa watu wanaokiulizia.
"Aisee kile kitabu changu nimeshakiingiza sokoni, na huwezi kuamini kimekuwa kikinukuliwa kama njugu tofauti na matarajio yangu, hali inayonifariji mno," alisema Assosa.
Mkongwe huyo aliyewahi kuzipigia bendi za Negro Succes, Orchestre Lipualipua, Fukafuka, Le Kamalee, Marquiz du Zaire, Marquiz Original, Mambo Bado, Legho Stars na sasa Bana Marquiz, alisema hakutaraji kama kingegombewa.
Alisema hakuwa na tumaini la kugombewa kwa kitabu chake kutokana na ukweli ndicho cha kwanza kwake kukitoa tangu aamue kujikita kwenye uandikaji wa vitabu, nje ya shughuli zake za muziki anaoendelea nao hadi sasa.
Aliongeza kuwa, hali hiyo unamfanya afikirie kuongeza idadi ya nakala zake, ili kukidhi mahitaji ya mashabiki wanaokiulizia ambacho ndani yake pia kina picha za wasanii wakongwe wa Kongo pamoja na yeye na familia yake.
"Kama watakuwa wanavihitaji pia wanaweza kwenda pale Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, kuna wakala anaviuza pale, au wanipigie katika 0713-240735, wanaweza kukipata," alisema Assosa.
Cloud atambia Basilisa
MSANII nyota wa filamu nchini, Issa Mussa 'Cloud', amedai filamu yake mpya ya 'Basilisa' ni funika bovu, miongoni mwa kazi zake alizowahi kuzitoa kwa hivi karibuni.
Cloud, alisema filamu hiyo iliowashirikisha wasanii kadhaa mahiri nchini, akiwemo mrembo Wema Sepetu na Ummy Wenslaunce 'Dokii', inaweza kuwa kazi bomba kwa mwaka huu wa 2011 kwa jinsi ilivyoandaliwa kwa ustadi mkubwa.
Mkali huyo aliyetamba na michezo ya kuigiza kupitia runinga kabla ya kuibukia filamu, alisema 'Basilisa' ambayo itasambazwa na kampuni ya Steps Entertainment ni bora kati ya zote alizowahi kuzitoa tangu aiingie kwenye fani hiyo.
Alisema kinachomfanya aamini hivyo ni kwa jinsi hadhithi yake ilivyo, namna alivyoshiriki na umahiri ulioonyeshwa na wasanii wenzake, acha upigaji picha wa kiwango cha hali juu na mandhari iliyotumika kurekodiwa kazi hiyo.
"Sio vibaya mtu kujisifia kwa jinsi anavyofanya kazi yake, nami naiona 'Basilisa' ni moja ya kati niliyoumiza kichwa na kushiriki kwa kiwango kikubwa, nadhani itakuwa miongoni mwa kazi bora kwa mwaka," alisema Cloud.
Msanii huyo, ambaye hushirikishwa kazi mbalimbali, alisema ndani ya filamu hiyo ameigiza katika nafasi tatu tofauti kama alivyowahi kufanya muigizaji wa Kimarekani, Eddy Murphy katika filamu yake ya 'Nutty Professor'.
Tofauti na Murphy aliyeigiza kikomedi zaidi, Cloud ndani ya filamu yake ameigiza 'siriazi' akiwa kama chizi, kiumbe wa kutisha na hali yake ya kawaida, kiasi ni vigumu kubaini kama nafasi hizo tatu tofauti zimechezwa na mtu mmoja.
Mbali na yeye (Cloud) wengine walioshiriki filamu hiyo itakayoingia sokoni mwezi ujao ni Adam Kuambiana, Dokii, Wema Sepetu, Selemani Barafu 'Mzee wa Land Rover', Single Mtambalike 'Richie', Kajala Masanja na wengineo.

Tuesday, April 19, 2011
Mama amtoa Hemed kwenye fani ya filamu
Msanii mkali wa filamu nchini, Hemed Suleiman 'PHD' yu mbioni kuachana na fani hiyo kwa muda ili akajikite kwenye masuala ya masomo.
Habari za chini ya kapeni zinasema kuwa, PHD, amelazimika kuachana na fani hiyo kwa sababu ya shinikizo la mama yake anayemuona kama anapotoka kushughulika na filamu, hadi kwanza achimbe kitabu.
PHD amefunguka mwenyewe akisema kuwa, atafanya kazi nne za mwisho mwisho kabla ya kuingia darasani, kati ya kazi hizo mbili ni zake binafsi na mbili ni za watu wengine ambazo alishaingia mkataba wa kuzifanyia kazi.
Hata hivyo amewasihi mashabiki wake kuwa, sio kama anasema kimoja, bali ni katika hali ya kuwatii wazazi kama vitabu vinavyosema 'Wafanyie Wema na Kuwatii Wazazi ili Mungu Akuzidishie Neema'

Sunday, April 10, 2011
Huba yaja na Bangkok Deal
Baada ya kutamba na filamu za Hazina na zile tulizorekodia watu wengine, kampuni yetu imeachia kazi mpya iitwayo Bangkok Deal ambayo tayari ipo madukani, ikisambazwa na kampuni ya Kapico Tanzania.
Ndani ya picha hii utashuhudia kisa cha deal lililoletwa toka Thailand la kusaka nyoka na kuibua kizaazaa cha aina yake.
Isake mwenyewe upate uhondo
Ndani ya picha hii utashuhudia kisa cha deal lililoletwa toka Thailand la kusaka nyoka na kuibua kizaazaa cha aina yake.
Isake mwenyewe upate uhondo
Subscribe to:
Posts (Atom)